Sheikh Hussein Mosh Abdullah i alieleza kuwa, kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, ndoa inaleta baraka, upendo, na mshikamano wa familia, na ni njia ya kujiepusha na maovu katika jamii. Aidha, aliwahimiza wanandoa kuijenga misingi ya ndoa yao juu ya heshima, subira, mawasiliano mazuri, na kumcha Mungu katika kila hatua ya maisha yao.

Shirika Ia Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Katika mwendelezo wa harakati za kuimarisha maadili ya kifamilia katika jamii ya Kiislamu, hafla ya ndoa ya Kiislamu imefanyika katika Mkoa wa Kigoma, Kijiji cha Kasuku, ikihudhuriwa na waumini pamoja na viongozi wa dini.
Katika hafla hiyo, Sheikh Hussein Moshi alitoa nasaha kwa wanandoa wapya na Waislamu kwa ujumla, akisisitiza kwamba ndoa ni Sunna njema na nguzo muhimu katika Uislamu. Alibainisha kuwa ndoa ndiyo msingi wa ustawi wa jamii, hifadhi ya maadili, na chanzo cha utulivu wa moyo kwa mwanamume na mwanamke.

Sheikh Moshi alieleza kuwa, kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, ndoa inaleta baraka, upendo, na mshikamano wa familia, na ni njia ya kujiepusha na maovu katika jamii. Aidha, aliwahimiza wanandoa kuijenga misingi ya ndoa yao juu ya heshima, subira, mawasiliano mazuri, na kumcha Mungu katika kila hatua ya maisha yao.

Waumini waliohudhuria hafla hiyo walipokea ujumbe huo kwa furaha, huku wakieleza kufurahishwa na kukua kwa shughuli za kidini katika kijiji cha Kasuku. Karibuni sana Kasuku, kwenye Nuru ya Ahlul Bayt (a.s).
Your Comment